mzeiya
Elder Lister
Mamlaka nchini Sri Lanka zimesema zimepata jiwe kubwa zaidi la thamani ya mamilioni ya pesa aina ya sapphire bila kutarajia .
Mfanyabiashara wa vito alisema jiwe hilo lilipatikana na wafanyikazi wakichimba kisima nyumbani kwake katika eneo lenye utajiri wa madini la Ratnapura.
Wataalam wanasema jiwe hilo, ambalo lina rangi ya samawati, lina thamani inayokadiriwa kufikia dola milioni 100 katika soko la kimataifa.
Jiwe hilo lina uzani wa karibu kilo 510 au karati milioni 2.5 na limepewa jina la "Serendipity Sapphire".
"Mtu ambaye alikuwa akichimba kisima hicho alitujulisha juu ya jiwe la kipekee. Baadaye baadaye tulipata jiwe hili la thamani kubwa," Bwana Gamage, mmiliki wa jiwe hilo, aliambia BBC.
Hakutaka kutoa jina lake kamili au eneo kwa sababu za usalama.
Bwana Gamage, ambaye ni mfanyabiashara wa vito wa kizazi cha tatu, alijulisha mamlaka juu ya ugunduzi huo, lakini ilichukua zaidi ya mwaka mmoja kusafisha jiwe kuondoa matope na uchafu mwingine kabla hawajalichambua na kulithibitisha.
Wakati wa mchakato wa kusafisha, Bw Gamage alisema mawe mengine yalitoka yalidondok na yaligunduliwa kuwa yakuti ya ubora wa juu.
Ratnapura, ambayo inamaanisha jiji la vito katika Sinhalese, unajulikana kama mji mkuu wa madini katika nchi hiyo Asia Kusini. Mawe mengine ya thamani yamepatikana huko zamani.
Sri Lanka ni muuzaji mkuu wa vito vingine vya thamani.
Mwaka jana, nchi hito ilipata karibu nusu bilioni ya dola kupitia uuzaji wa kigeniwa vito naalmasi
"Sijawahi kuona jiwe kubwa la thmani kama kama hilo hapo awali. Hii labda iliundwa karibu miaka milioni 400 iliyopita," Dk Gamini Zoysa, mtaalam mashuhuri wa jiolojia aliambia BBC.
Wataalam pia wanasema hata hivyo, kwamba ingawa jiwe holo lina thamani kubwa ya karati, mawe yote ndani yake hayawezi kuwa ya ubora wa hali ya juu .
Utaftaji huo unakuja wakati tasnia ya vito ya Sri Lanka imepata hasara kwa sababu ya janga la Corona .
Wale wanaofanya kazi katika sekta hiyo wanatumai "Jiwe la Serendipity" sasa litavutia wanunuzi na wataalam wa kimataifa - ingawa jiwe hilo bado halijachambuliwa na kuthibitishwa na wataalam huru wa kimataifa.
"Ni jiwe la thamani , labda ndio kubwa zaidi ulimwenguni. Kwa ukubwa na thamani yake, tunafikiria itavutia wauzaji wa vito na madini au majumba ya kumbukumbu," Thilak Weerasinghe, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Vito nchini Sri Lanka, anasema.